Monday, September 22, 2014

PELLEGRINI AIPONDA CHELSEA KWA KUPAKI BASI.

MENEJA wa klabu ya Manchester City, Manuel Pellegrini ameiponda Chelsea kwa kucheza kama timu ndogo wakati timu hizo zilipotoka sare ya kufungana bao 1-1 katika mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa katika Uwanja wa Etihad jana. Nyota wa Chelsea Andre Schurrle ndio aliyeifungia Chelsea baop la kuongoza kabla ya Feank Lampard aliyetokea benchi kuisawazishia Cioty bao hilo. Akihojiwa Pellegrini amesema wapinzani wao Chelsea walicheza kama timu ndogo kwani muda mwingi walikuwa wakijihami badala ya kucheza mpira. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa sio jambo zuri kamwe wakati timu moja inapofanya kazi ya kuzuia kwani kunakuwa hakuna ladha ya soka.

No comments:

Post a Comment