Friday, September 19, 2014

MWENYEKITI WA FA ATANGAZA KURUDISHA SAA YA KIFAHARI ALIYOPEWA NA CBF.

MWENYEKITI wa Chama cha Soka nchjini Uingereza-FA Greg Dyke amesema atarudisha saa ya kifahari aliyopewa na Shirikisho la Soka la Brazil-CBF. Shirikisho la Soka Duniani-FIFA limeagiza maofisa kurudisha saa hizo ambazo zinadiriwa kuwa na thamani ya paundi 16,000 au wajiweke katika hatari ya kuchukulia hatua za kinidhamu. Zawadi hizo za kumbukumbu zilitolewa na wadhamini wa CBF kwa watu kadhaa katika Kombe la Dunia wakiwemo wajumbe 28 wa kamati ya utendaji ya FIFA. Akihojiwa kuhusiana na hilo Dyke amesema wanachukua hatua ya kurudisha begi hilo la zawadi pamoja na vitu vilivyomo ndani yake ambavyo bado vipo kama vilipangwa awali. Saa hizo za kifahari walipewa maofisa wa vyama 32 vya soka kwa nchi zilizoshiriki Kombe la Dunia, wajumbe 28 wa kamati ya utendaji ya FIFA na tano zingine kwa wajumbe wa vyama vya soka kwa nchi za Amerika Kusini.

No comments:

Post a Comment