Friday, September 19, 2014

YAYA TOURE NDIO ANAYEIGHARIMU CITY - SCHOLES.

KIUNGO wa zamani wa klabu ya Manchester United amesema nyota wa Manchester City Yaya Toure ndio tatizo kuwa kwa mabingwa hao wa Ligi Kuu katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kiungo huyo wa kimataifa wa Ivory Coast alishindwa kuwazuia Bayern Munich wakati kikosi cha Pep Guardiola kilishinda bao 1-0 huko Allianz Arena Jumatano usiku na Scholes anaamini kuwa uwezo wa mdogo wa kuzuia wa Toure ndio chanzo cha kufungwa kwao. Scholes amesema anadhani habari ni ile ile katika michuano hiyo kwa City kwani Yaya Toure kushindwa kuzuia kumekuwa tatizo kubwa kwao. Nyota huyo ameendelea kudai kuwa kushindwa kuzuia kwa Toure kumekuwa kukimpa kazi kubwa Fernandinho kwani amekuwa akifanya kazi za watu wawili kwa wakati mmoja. Scholes ameendelea kwa kushauri kuwa kama wakifanikiwa kutinga hatua ya timu 16 bora msimu huu, City watapaswa kutumia viungo wawili wa kukaba ambao wanaweza kuwa tayari kucheza nyuma badala ya kutumia kiungo mmoja.

No comments:

Post a Comment