Monday, September 29, 2014

ROONEY AOMBA RADHI KWA KADI NYEKUNDU ALIYOPEWA.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Manchester United, Wayne Rooney amewaomba radhi wachezaji wenzake kwa kadi nyekundu aliyopewa katika mchezo dhidi ya West Ham United uliochezwa Jumamosi iliyopita. Nahodha huyo wa United alitolewa baada kumkwatua kwa makusudi mchezaji wa West Ham Stewart Downing na amedai kuwa hatakata rufani kupinga uamuzi wa mwamuzi Lee Mason aliyechezesha mchezo huo. Akihojiwa Rooney amesema alifanya mahesabu yake vibaya kwani alidhani mchezaji huyo anaweza kuleta madhara katika lango lao lakini haikuwa hivyo ndio maana anaomba radhi. Katika mchezo huo United ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 pamoja na kucheza wakiwa pungufu kwa muda wa dakika 30. Rooney sasa hataitumikia United ka michezo mitatu mpaka Novemba 2 mwaka huu wakati watakapokwaana na mahasimu wao Manchester City. 


No comments:

Post a Comment