Friday, September 26, 2014

SIMBA, YANGA SASA KUKIPIGA OCTOBA 18.

MCHEZO wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaowakutanisha watani wa jadi Yanga na Simba umesogezwa mbele mpaka Octoba 18 mwaka huu kutokana na ratiba ya ligi kufanyiwa marekebisho. Ratiba hiyo ambayo hapo awali ilielekeza mchezo huo kuchezwa Octoba 12 sasa imesogezwa mbele ili kupisha ratiba ya mechi za kimataifa ambayo iko katika kalenda ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA. Badala ya mchezo huo sasa timu ya taifa ya Tanzania-Taifa Stars itaivaa Benin katika mchezo wa kirafiki utakaochezwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mbali na mchezo huo mechi zingine zote ambazo zilikuwa zichezwe tarehe hiyo na siku inayofuata sasa zitachezwa wikiendi inayofuata ya Octoba 18 na 19.

No comments:

Post a Comment