KIUNGO mkongwe wa Barcelona Xavi Hernandez ameweka wazi kuwa hadhani kama ataweza kucheza katika timu nyingine na amepania kumaliza kabisa soka lake akiwa hapo. Kiungo alikuwa akihusishwa na tetesi za kuondoka Camp Nou katika kipindi cha usajili wa majira ya kiangazi huku Manchester United na Bayern Munich zikitajwa kuiwinda saini yake sambamba na vilabu kutoka Qatar na Ligi Kuu ya Soka nchini Marekani. Hata hivyo, Xavi amekiri kuwa anaona uzito kuondoka katika timu hiyo ambayo ameichezea katika kipindi chake chote. Xavi mwenye umri wa miaka 34 amesema kama ni amri yake asingweza kuondoka katika timu hiyo kwani alikuwa akitaka kuondoka mara nyingi lakini alishindwa kutokana na mapenzi aliyonayo. Kiungo amesema tayari ameshaufahamisha uongozi kuwa hana mpango wowote wa kucheza katika klabu nyingine hivyo sasa waliobaki ni wao kuamua kabla ya mkatab wake haujamalizika Juni mwaka 2016.
No comments:
Post a Comment