MSHAMBULIAJI wa klabu ya Manchester United, Wayne Rooney amemmwagia sifa meneja wake wa zamani Sir Alex Ferguson kwa kudai kuwa ni kocha bora kabisa kuwahi kutokea. Rooney mwenye umri wa miaka 28 alitua Old Trafford mwaka 2004 baada ya Ferguson kumsajili kutoka Everton kwa kitita cha paundi milioni 25.6 wakati akiwa bado kinda. Pamoja na uhusiano baina ya wawili kuyumba mara kadhaa huko nyuma, Rooney amekiri Ferguson ambaye aliisaidia United kushinda mataji 13 ya Ligi Kuu, matano ya Kombe la FA na moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya ataendelea kuhamasisha vizazi katika klabu hiyo. Akihojiwa Rooney amesema alitua Old Trafford akiwa kijana mdogo na alikutana wenzake wachache kama yeye ambapo Ferguson aliwakuza na kuwafanya kuwa wachezaji bora kabisa. Rooney aliendelea kudai kuwa anashukuru kwa kila kitu ambacho Ferguson amemfanyia na anadhani ndio kocha bora kabisa aliyewahi kutokea katika klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment