WACHEZAJI nyota Clint Dempsey na Obafemi Martins wamefanikiwa kuingoza klabu ya Seattle Sounders kushinda taji lao la nne la michuano ya Kombe la Marekani baada ya kufunga katika dakika za nyongeza na kuifanya timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Philadelphia Union. Dempsey ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Marekani alifunga bao lake katika dakika ya 11 ya muda wa nyongeza kabla ya Martins hajaongeza bao lingine dakika nne baadae. Klabu hiyo pia imefanikiwa kushinda taji hilo mara tatu mfululizo kuwanzi mwaka 2009 mpaka 2011, huku wakijihakikishia nafasi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa kwa nchi za CONCACAF. Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Philadelphia kucheza fainali ya kwanza ya michuano hiyo katika historia ya miaka mitano ya klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment