Wednesday, September 17, 2014

QUEIROZ AULA TENA IRAN.

SHIRIKISHO la Soka nchini Iran hatimaye limeamua kumuongeza mkataba wa miaka minne kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo Carlos Queiroz. Kocha huyo wa zamani wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno alikuwa amesema ataachia ngazi baada ya kutolewa katika michuano ya Kombe la Dunia Juni mwaka huu akidai kutolewana na baadhi ya viongozi wa shirikisho la nchi hiyo. Lakini baada ya kufanyika kwa mazungumzo Queiroz alikuwa mkataba mwingine wa miaka minne kuendelea kuinoa timu hiyo huku changamoto yake ya kwanza ikiwa ni kuhakikisha wanafanya vyema katika michuano ya Kombe la Asia. Akihojiwa mara baada ya makuabaliano hayo Queiroz amesema lengo lao la kwanza kuhakikisha wanafanya vyema katika michuano ya Asia Januari mwakani huku lengo lao la pili likiwa ni kuhakikisha wanafuzu michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018. Iran wamepangwa katika kundi C katika michuano ya Asia sambamba na nchi za Muungano wa falme za kiarabu-UAE, Bahrain na Qatar.

No comments:

Post a Comment