SHIRIKISHO la Soka barani Afrika-CAF limeitaka klabu ya Entente Setif ya Algeria kucheza mchezo wao wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe bila kuwepo mashabiki. Setif inatarajia kuwa mwenyeji wa Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC Septemba 20 mwaka huu. CAF imefikia uamuzi wa kuwafungia mashabiki wa klabu hiyo kufuatia tabia yao isiyokuwa ya kimichezo ambayo wamekuwa wakiirudia mara kwa mara. Hatua hiyo imefikiwa kufuatia ripoti kadhaa ambazo zimekuwa zikitolewa na waamuzi kususani katika mechi za hatua ya makundi.
No comments:
Post a Comment