CHAMA cha Soka nchini Uingereza-FA kimetoa rasimu ya kwanza ya mapendekezo ya kupunguza idadi ya wachezaji walio nje ya Muungano wa Ulaya kwa asilimia 50. Mapema mwaka huu tume ya FA ilitoa wito wa kufanyika mabadiliko ya jumla kwa imani kwamba vilabu vimekuwa vikinunua wachezaji wa kigeni. Mabadiliko hayo ya sheria inayopendekezwa tayari yametumwa katika Ligi Kuu, Ligi za Chini na vyama vya umoja wa wachezaji na makocha. FA ina matumaini kuwa mfumo huo unaweza kuanza kufanya kazi katika msimu wa 2015-2016. FA ina matumaini ya kutuma rasimu ya makubaliano ya mabadiliko kwa mawaziri wa serikali kabla ya mwaka kumalizika. Lengo kubwa ya FA kupunguza wachezaji wa kigeni ni kuongeza idadi ya wachezaji chupukizi nchini humo kwani wanaamini kuwa wingi wa wachezaji wa kigeni unazuia nafasi kwa wachezaji wazawa kupatanafasi.
No comments:
Post a Comment