Wednesday, September 17, 2014

LIVERPOOL BADO - GERRARD.

NAHODHA wa klabu ya Liverpool, Steven Gerrard amesema timu hiyo inapaswa kuimarika ili iweze kusonga mbele katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kupata penati katika dakika za mwisho iliyowafanya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ludogorents ya Bulgaria. Liverpool mabingwa wa michuano hiyo mwaka 2005, waliokaribia kugawana alama na wapinzani wao hao ambao walikuwa hawapewi nafasi wakati Dani Abalo aliposawazisha bao baada ya Mario Balotelli kufunga bao la kuongoza. Lakini penati iliyopigwa na Steven Gerrard iliihakikishia udhindi Liverpool ambao watasafiri kuifuata FC Basel katika mchezo unaofuata kabla ya kuwakaribisha Real Madrid nyumbani. Akihojiwa Gerrard amesema walifanya vyema katika mchezo lakini sio vyema sana hiovyo wanapaswa kujitahidi zaidi ili waweze kuimarika kabla ya kukutana na Madrid. Mbali na Gerrard, meneja wa timu hiyo Brendan Rodgers naye amekiri kikosi chake kinahitaji kutafuta makali yao baada ya kuanza msimu kwa kusuasua.

No comments:

Post a Comment