Wednesday, September 17, 2014

BENZEMA AMFUNGA MDOMO ZIDANE.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Real Madrid, Karim Benzema amesisitiza kuwa ushindi ni muhimu zaidi kwake kuliko kufunga wakati timu hiyo ilipoisambaratisha FC Basel kwa mabao 5-1 katika mchezowa Ligi ya Mabingwa Ulaya uliochezwa Uwanja wa Santiago Bernabeu jana usiku. Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa amekuwa akikosolea kiwango chake katika wiki za karibuni mojawapo akiwa kocha wa timu B Zinedine Zidane ambaye alimtaka mchezaji huyo kuongeza makali yake ya kufunga. Hata hivyo, Benzema aliwanyamazisha wanaomkosoa kwa bao alilofunga katika dakika ya 79 ya mchezo huo likiwa ni bao 1,000 kwa timu hiyo katika michuano hiyo. Akihojiwa Benzema amesema amefurahi sana kwamba amefunga katika mchezo huo lakini ushindi ndio muhimu zaidi kwake. Benzema amesema timu hiyo ilikuwa imepita katika kipindi kigumu kabla ya mchezo huo hivyo ushindi lilikuwa jambo muhimu ili kuwarejeshea hali yao ya kujiamini. Jumamosi hii Madrid watakuwa na kibarua kingine wakati watakapokuwa wageni wa Deportivo La Coruna katika mchezo wa La Liga.

No comments:

Post a Comment