Wednesday, September 17, 2014

WENGER AMKINGIA KIFUA WELBECK.

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesema mashabiki wanapaswa kua wavumilivu na mchezaji mpya aliyesajiliwa Danny Welbeck baada kukosa bao ambalo inadhaniwa ndio lililoigharimu timu hiyo kufungwa mabao 2-0 na Borussia Dortmund katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 23 ambaye alitua Arsenal akitokea Manchester United kwa kitita cha paundi milioni 16, alikosa bao la wazi katika mchezo huo wa kundi wakati timu hizo zikiwa bado hazijafungana. Baadae Dortmund walifunga bao dakika za mwisho kabla ya muda wa mapuimziko na kuongeza lingine katika kipindi cha pili na kujihakikishia alama zote tatu katika mchezo huo. Akihojiwa Wenger amesema ana uhakika Welbeck ataimarika hivyo hawapaswi kuwa na shaka na hilo pamoja na kukosa nafasi kama tatu za kufunga. Wenger aliendela kudai kuwa Welbeck alicheza vyema katika kipindi cha kwanza huku akikosa nafasi kadhaa lakini wanachopaswa kufanya ni kuwa subira kwani anaamini nyota huyo ataimarika kadri siku zinavyokwenda. Welbeck alifunga mabao amwili wakati Uingereza ikiitandika Switzerland kwa mabao 2-0 katika mechi za kufuzu michuano ya Ulaya Septemba 8 lakini kwa klabu vyota huyo hajafunga bao toka alipofunga katika Ligi Kuu wakati United ilipoifunga West Bromwich Albion mabao 3-0 Machi mwaka huu. Arsenal sasa inakabiliwa na mchezo mwingine wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Galatasaray katika Uwanja wa Emirates Octoba mosi mwaka huu.

No comments:

Post a Comment