WINGA wa klabu ya Newcastle United Jonas Gutierrez amebainisha kuwa anaendelea na matibabu ya saratani ya korodani nchini kwake Argentina. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 31 ambaye mara ya mwisho kucheza ilikuwa Aprili mwaka huu wakati akiwa kwa mkopo katika klabu ya Norwich City, alirejea Amerika Kusini wakati alipogundulika na ugonjwa huo na alifanyiwa upasuaji ya kuondoa kokwa la upande wa kushoto wa korodani. Akihojiwa Gutierrez amesema wakati alipothibitisha kwamba ana saratani alirudi nyumbani na kuanza kulia kwani alijua huo ni mchezo mgumu ambao atatakiwa kucheza. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa baada ya kufanyiwa upasuaji sasa anaendelea na matibabu ya kidini au chemotherapy. Gutierrez amesema ameamua kuelezea habari yake kwasababu anadhani inaweza kuwasaidia watu wengine ambao wana saratani.
No comments:
Post a Comment