Wednesday, September 17, 2014

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: LIVERPOOL, MADRID, MONACO KIDEDEA, ARSENAL, ATLETICO WAANGUKIA PUA.

MICHUANO ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya imeanza kutimua vumbi rasmi jana usiku kwa timu kadhaa kushuka viwanjani kutafuta alama tatu muhimu ili kuwaweka sawa katika makundi yao. Mabingwa watetezi wa michuano hiyo Real Madrid wao waliwaalika FC Basel katika Uwanja wa Santiago Bernabeu ambapo bila ya huruma waliwachakaza wenyeji wao hao mabao 5-1 huku washambuliaji wake Karim Benzema, Gareth Bale, Cristiano Ronaldo na James Rodriguez wote wakifunga kwenye mchezo huo. Kwa upande mwingine Liverpool ambao wameingia katika michuano hiyo kwa mara ya kwanza baada ya kupita miaka mitano walifanikiwa kuutumia vyema uwanja wao wa nyumbani wa Anfield kwa kuitandika Ludogorets Razgrad kwa mabao 2-1. Katika michezo mingine iliyochezwa jana mambo hayakuwa mazuri sana kwa Atletico Madrid ambao msimu uliopita walitinga fainali ya michuano hiyo baada ya kukubalia kipigo cha mabao 3-2 kutoka kwa wenyeji wao Olympiakos. Kwingine Arsenal ilishindwa kutamba ugenini baada ya kutandikwa na Borussia Dortmund kwa mabao 2-0, Benfica walishindwa kutumia uwanja wao wa nyumbani baada ya kutandikwa na wageni wao Zenit St. Petersburgmabao 2-0, Monaco ilishinda bao 1-0 na Galatasaray ilishindwa kutambiana na Anderlecht kwa kufungana bao 1-1. Michuano hiyo inaendelea tena leo ambapo mashabiki wengi wanausubiria mchezo utakaowakutanisha mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich watakaochuana na mabingwa wa Uingereza Manchester City huko Allianz Arena.

No comments:

Post a Comment