Friday, September 26, 2014

SUAREZ AITWA URUGUAY.

LUIS Suarez amekuwa mmoja kati ya wachezaji 29 walioitwa katika kikosi cha awali cha timu ya taifa ya Ureno kwa ajili ya mechi za kirafiki mwezi ujao dhidi ya Saudi Arabia na Oman. Kocha wa timu hiyo Oscar Tabarez bado atahitajika kuamua kama atamchukua Suarez kwa ajili ya michezo hiyo ambapo mmoja dhidi ya Saudi Arabia utachezwa Octoba 10 huku ule dhidi ya Oman ukichezwa siku tatu baadae. Suarez yuko anatumikia adhabu ya mechi nane za kimataifa kwa kosa la kumng’ata Giorgio Chiellini katika Kombe la Dunia, hivyo inamaanisha kuwa atakosa michuano ya Copa Amerika mwakani na baadhi ya mechi za kufuzu Kombe la Dunia 2018. Adhabu hiyo hiyo inamzuia kucheuia kucheza mechi za mashindano katika klabu yake ya Barcelona mpaka mwezi ujao. Tabarez hakumuita Suarez katika mechi mbili za kirafiki zilizochezwa mwezi huu dhidi ya Japan na Korea Kusini ambazo zote Uruguay ilishinda.

No comments:

Post a Comment