Friday, September 26, 2014

LAMPARD AKANUSHA KUFANYA MAZUNGUMZO NA CITY.

KIUNGO mkongwe wa klabu ya Manchester City, Frank Lampard amesema hajafanya mazungumzo yoyote na klabu hiyo kuhusu kuongeza muda wake wa mkopo. Kiungo huyo wa zamani wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 36 amefunga mabao matatu katika katika mechi tatu alizoichezea City toka ajiunge nao kipindi hiki cha kiangazi akitokea timu ya New Yorkl City inayoshiriki Ligi Kuu nchini Marekani-MLS. Mkataba wa mkopo wa Lampard unatarajiwa kumalizika Januari lakini meneja wa City Manuel Pellegrini alikaririwa mapema wiki hii kuwa anaweza kuendelea kuwepo. Akiulizwa kuhusu suala hilo, Lampard amesema kwasasa hawezi kusema kusema chochote kuhusu kuendelea kwani anachojua mkataba wake unamalizika Januari. Lampard ambaye alistaafi soka la kimataifa Agosti baada ya kuitumikia nchi yake kwa michezo 106, alicheza mechi yake ya kwanza akiwa na City katika sare ya mabao 2-2 dhidi ya Arsenal Septemba 13 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment