Friday, September 26, 2014

RUFANI YA KABYLIE YATUPWA.

Albert Ebosse
KAMATI ya nidhamu ya Shirikisho la Soka la Algeria imetupilia mbali rufani ya klabu ya JS Kabylie kupunguza adhabu waliyopewa kufuatia kutopkea kwa kifi kwa mchezaji wa kimataifa wa Cameroon Albert Ebosse katika uwanja wao wa nyumbani mwezi uliopita. Kabylie walikutwa na hatia ya uzembe baada ya tukio hilo lililotokea katika Uwanja wa Novemba 1st uliopo huko Tizo Ouzou ambapo walifungiwa kutumia uwanja huo mpaka watakapopewa taarifa vinginevyo. Klabu hiyo yenye maskani yake kaskazini mwa Algeria pia itacheza mechi zake za nyumbani za ligi zilizosalia katika uwanja huru na bila kuwa na mashabiki. Uongozi wa klabu hiyo sasa umedai kuwa utapeleka suala hilo katika mahakama ya michezo ya nchi hiyo. Ebosse alitandikwa na kitu kizito kichwani kilichoruswa na shabiki mwenye hasira wakati wachezaji wa Kabylie akitoka uwanjani baada ya kufungwa na USM Alger mabao 2-1 Agosti 23 mwaka huu. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alifariki saa chache baadae akiwa hospitalini kufuatia damua kuganda katika ubongo kutokana na tukio hilo.

No comments:

Post a Comment