Friday, September 26, 2014

APPIAH AELEZA MADUDU YA PRINCE BOATENG.

HATIMAYE aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Ghana Kwesi Appiah amezungumza sababu zilizomfanya kumtimua katika kikosi chake Kevin-Prince Boateng katika kambi ya timu hiyo nchini Brazil. Uamuzi wa kumtimua kiungo huyo wa klabu ya Schalke na kiungo wa AC Milan Suley Muntari uliteka vyombo vya habari vya kimataifa na Appiah amesema alifanya hivyo kwasababu ya kutokuwa mfano wa kuigwa kwa wenzake. Appiah amesema Boateng mara kadhaa amekuwa akitumia lugha ya matusi mazoezini na muda mwingi amekuwa akinyamaza kimya na kujifanya hakusikia. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa aliamua kufikia uamuzi wa kumtimua baada ya kuelekeza matusi hayo moja kwa moja kwake na mengine kwa viongozi wenzake wa benchi la ufundi. Appiah amesema alikuwa hana nia ya kumuondoa lakini wakati alipotoa matusi hayo mbele ya wachezaji wenzake akaona hana jinsi kwani alikuwa analeta mfano mbaya mbele ya wachezaji wadogo.

No comments:

Post a Comment