Tuesday, September 23, 2014

SUAREZ KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI YA KIKOSI B CHA BARCELONA.

MENEJA wa Barcelona, Luis Enrique amethibitisha kuwa Luis Suarez atacheza katika kikosi B cha timu hiyo katika mchezo wao wa kirafiki dhidi ya timu ya vijana na Indonesia kesho. Nyota huyo wa kimataifa wa Uruguay alisajiliwa Barcelona kwa kitita cha euro milioni 88 Julai lakini bado hajapata nafasi ya kucheza kutokana na kutumikia adhabu ya kufungiwa miezi minne kwa kumng’ata Giorgio Chiellini ambapo adhabu inatarajiwa kumalizika Octoba 25 mwaka huu. Hata hivyo, Enrique amebainisha kuwa atamchezesha mshambuliaji huyo ili kumpa mazoezi kabla ya kurejea katika kikosi cha kwanza pindi atakapomaliza adhabu yake. Kocha huyo amesema ni jambo jema kwa Suarez kucheza kwani anakuwa ajiweka fiti tayari kwa mechi baada ya kukaa nje kwa muda mrefu bila kucheza mechi ya mashindano. Wakati Suarez akitarajia kucheza katika kikosi B hapo kesho, wachezaji wenzake wa kikosi cha kwanza watasafiri kuifuata Malaga huku wakiwa na matumaini ya kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa La Liga.

No comments:

Post a Comment