Tuesday, September 23, 2014

LIVERPOOL YARUHUSIWA KUUTANUA UWANJA WA ANFIELD.

KLABU ya Liverpool imepewa ruhusa ya kutanua Uwanja wa Anfield kutokana uwezo wa kubeba mashabiki 45,500 mpaka 59,000 ikiwa ni sehemu ya mpango utakaogharimu kiasi cha paundi milioni 100. Kamati ya mipango ya halmashauri ya mji wa Liverpool imepitisha mpango wa kutanua jukwaani kubwa kwa viti 8,300 na jukwaa linatizama barabara kwa viti 4,800. Mapendekezo hayo yamejumuisha ukumbi wa mikutano na sehemu za kutunzia vifaa, maduka mapya na eneo la ziada la kuegesha magari. Ujenzi wa upanuzi unatarajiwa kuanza rasmi mwakani huku ukitarajiwa kukamilika msimu wa 2016-2017. Mpango huo utaifanya klabu hiyo kuweza kuandaa mechi za kimataifa sambamba na mechi za Ulaya. Uwanja wa Anfield ulifungiliwa rasmi mwaka 1884 ukiwa na uwezo wa kuingiza mashabiki 20,000 na ulikuwa ukitumiwa na timu ya Everton mpaka walipoondoka na kwenda katika Uwanja wao wa Goodison Park na klabu ya Liverpool ilipoanzishwa mwaka 1892 ndio ikachukua uwanja huo.

No comments:

Post a Comment