Tuesday, September 23, 2014

SANTOS ATEULIWA KUWA KOCHA WA URENO.

SHIRIKISHO la Soka nchini Ureno, FPF limemteua Fernando Santos kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya nchi hiyo. Katika taarifa ya FPF iliyotumwa katika mtandao ilithibitisha habari hiyo ya kumuajiri Santos ambaye alikuwa akiinoa timu ya taifa ya Ugiriki hapo kabla. Santos ambaye aliingoza Ugiriki katika hatua ya timu 16 bora katika michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil ambapo walikuja kufungwa na Costa Rica kwa matuta anachukua nafasi ya Paulo bento aliyetimuliwa. Kibarua chake cha kwanza akiwa na Ureno, utakuwa mchezo unaiofuata wa kufuzu michuano ya Ulaya dhidi ya Denmark Octoba 14 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment