Tuesday, September 23, 2014

ESSIEN PANCHA TENA.

KIUNGO mahiri wa kimataifa wa Ghana, Michael Essien anatarajiwa kuwa nje kwa wiki mbili kutokana na majeruhi. Kiungo wa klabu ya AC Milan alipata majeraha ya mguu wakati wa maandalizi ya mchezo wa Serie A wa mwishoni mwa wiki iliyopita dhidi ya Juventus ambao walifungwa bao 1-0. Essien hatarajiwi kuwa sehemu ya kikosi cha wachezaji 23 watakaosafiri kwenda kupambana na Empoli. Nyota huyo amekuwa akiandamwa na majeruhi katika miezi ya karibuni kwani alishindwa kuitumikia vyema timu yake ya taifa kutoka matatizo ya majeruhi hatua am,bayo ilichangia kuondolewa mapema.

No comments:

Post a Comment