Tuesday, September 23, 2014

WALCOTT KUREJEA UWANJANI OCTOBA.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Uingereza, Theo Walcott anatarajiwa kurejea uwanjani tena uwanjani kuitumikia timu yake ya Arsenal Octoba baada ya kukaa nje kwa miezi 10 kutokana na majeruhi goti. Walcott anatarajiwa kurejea baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa ambapo Uingereza itacheza na San Marino Octoba 9 na Estonia siku tatu baadae. Walcott mwenye umri wa miaka 25 aliumia goti lake la kushoto wakati wa mchezo wa Kombe la FA mzunguko wa tatu dhidi ya Tottenham Hotspurs Januari mwaka huu. Majeruhi hayo yalipeleka kukosa michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika nchini Brazil. Kama akifanikiwa kurejea uwanjani mwezi ujao, anaweza kujumuishwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kitakachoachuana na Slovenia katika mchezo wa kufuzu michuano ya Ulaya Novemba 15.

No comments:

Post a Comment