Tuesday, September 23, 2014

MECHI ZA LIGI KUU UGANDA KUSIMAMA KWA DAKIKA KWA HESHIMA YA MCHEZAJI ALIYEAGA DUNIA AKITIZAMA MECHI CITY NA CHELSEA.

VILABU vinavyoshiriki Ligi Kuu nchini Uganda vinatarajia kusimama kwa dakika moja na kuvaa vitambaa vyeusi kabla ya kuanza kwa mechi zao wiki hii kwa heshima beki wa timu ya Simba Fahad Musana aliyefariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita. Musana mwenye umri wa miaka 24 alifariki dunia Jumapili wakati akitizama mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza kati ya Manchester City na Chelsea timu ambayo ni anaishabikia. Taarifa zinadai kuwa Musana ambaye alizikwa leo nyumbani kwake katika wilaya ya Iganga alifariki kwa shinikizo baada ya timu yake ya Chelsea kufungwa bao la kusawazisha dakika za mwisho wakati wengine wanadai alikuwa ameshafariki wakati Frank Lampard akiisawazishia City. Jambo lingine linalohusishwa na kifo cha mchezaji huyo ni katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Entebe uliochezwa Jumamosi iliyopita ambapo Musana aligongwa kichwani.

No comments:

Post a Comment