Tuesday, September 23, 2014

FIFA KUANZISHA MPANGO MPYA KUWALINDA ZAIDI WACHEZAJI.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA linatarajia kuwasilisha pendekezo katika kamati ya utendaji la kuangalia mbinu mpya za kukabiliana na majeraha ya kichwa. Kiongozi wa kamati ya tiba ya FIFA, Michel D’Hooghe aliandaa mpango huo mapema mwezi huu. Mpango huo unampa nafasi mwamuzi kusimamisha mchezo kwa dakika tatu ili daktari wa timu aweze kufanya tathmini yake uwanjani huku pia akipewa rungu la kuamua kama mchezaji anaweza kuendelea kucheza. Mapendekezo hayo yanafanana na taratibu mpya za Ligi Kuu zilizotolewa mwanzoni mwa msimu huu na ambazo pia ziliwasilishwa Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA Septemba 18 mwaka huu. Kama mapendekezo hayo yakipitishwa na FIFA na UEFA, yataanza kufanya kazi kuanzia Octoba na kujumuishwa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Europa League pamoja na mechi za kimataifa.

No comments:

Post a Comment