Tuesday, September 23, 2014

SINA SHAKA NA GERRARD - RODGERS.

MENEJA wa klabu ya Liverpool Brendan Rodgers amesisitiza kuwa hana mashaka na Steven Gerrard baada ya kupoteza michezo mitatu kati ya mitano ya Ligi Kuu waliyocheza msimu huu. Gerrard ambaye ni nahodha wa Liverpool alikuwa akihaha huku na kule katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya West ham United ili kuona uwezekano kama anaweza kubadilisha matokeo. Hata hivyo mambo hayakwenda kama walivyotarajia kwani mwisho wa mchezo walijikuta wamechapwa mabao 3-1 na timu hiyo. Rodgers amekaa kumshuhia lawama nahodha wake huyo kwa kudai kuwa kikosi kizima hakucheza vizuri katika mchezo huo waliopoteza. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa Gerrard bado ana mchango mkubwa sana kwa timu hiyo.

No comments:

Post a Comment