Thursday, September 25, 2014

TIMU YA KIKAPU YA WANAWAKE YA QATAR YAJITOA KATIKA MASHINDANO KWA KUNYIMWA KUVAA HIJAB.

TIMU ya taifa ya mpira wa kikapu ya wanawake ya Qatar imejitoa katika michuano ya Asia inayofanyika nchini Korea Kusini baada ya kukataliwa ombi lao la kutaka kuruhusiwa kutumia hijab wakati michuano hiyo. Wachezaji wa timu hiyo walitakiwa kuondoa vitambaa kichwani ambavyo hutumiwa na wanawake wa dini ya Kiislamu kabla ya mchezo dhidi ya Mongolia lakini walikataa na kupoteza mchezo huo. Sheria za mchezo huo duniani imeorodhesha kofia za kichwani na vibanio vya nywele kama vitu visivyotakiwa uwanjani. Huku kukiwa na hakuna dalili kwanza sheria hiyo inaweza kubadilishwa kabla ya mchezo wao unaofuata dhidi ya Nepal, timu hiyo imemua kujitoa. Michezo mingine katika mashindano hayo ya Asia yanaruhusu wanamichezo kuvaa hijab ambapo kilele chake kinatarajiwa kuwa Octoba 4 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment