MENEJA wa klabu ya Real Madrid, Carlo Ancelotti amekiri katika vyumba vya kubadilishia nguo kulikuwa na mgawanyiko wakati timu hiyo ilipokuwa chini ya kocha Jose Mourinho. Iliripotiwa kuwa Mourinho alikuwa na mgogoro na baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza wakati akiifundisha timu hiyo, ikiwemo suala la kutemeana mate katika uwanja mazoezi na Sergio Ramos na ia kushindwa kuelewana na nahodha Iker Casillas. Ancelotti sasa amebainisha kuwa kulikuwa na baadhi ya matatizo katika vyumba vya kubalishia nguo lakini amedai alikuwa hali ya amani alipowasili kuinoa timu hiyo. Kocha huyo amesema kabla ya hajakwenda Santiago Benarbeu alikuwa akifahamu uwa kulikuwa na matatizo kati ya wachezaji na Mourinho lakini alipochukua mikoba rasmi alikuwa hali ikiwa tulivu.

No comments:
Post a Comment