Friday, October 10, 2014

WATAALAMU WETU NDIO WATAKAOTOA USHAURI KUHUSU OZIL - WENGER.

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesema watapanga ratiba ya matibabu ya Mesut Ozil baada ya kiungo huyo kurejea kutoka katika majukumu ya kimataifa akiwa majeruhi. Ozil anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi mitatu kutokana na majeruhi ya goti baada ya kufanyiwa vipimo akiwa na timu ya taifa ya Ujerumani. Lakini Wenger amesema mtaalamu wa klabu hiyo ndio atakaetoa ushauri wa jinsi gani ya kukabiliana na tatizo hilo wakati watakapotafuta utaratibu wa kumtibu haraka iwezekanavyo. Wenger aliendelea kudai kuwa madaktari wa Arsenal nao wataangalia vipimo alivyofanyiwa na kutoa ushauri wao. Arsenal imeandamwa na majeruhi kadhaa msimu huu lakini Wenger amabinisha kuwa Theo Walcott na Serge Gnabry wote wanakaribia kurejea katika kikosi cha kwanza wakati Aaron Ramsey naye amebakisha siku nane kabla ya kuanza mazoezi.

No comments:

Post a Comment