Friday, October 10, 2014

BALE ANAWEZA KUFIKIA UBORA WA MESSI NA RONALDO - BEGOVIC.

GOLIKIPA wa kimataifa wa Bosnia- Hercegovina, Asmir Begovic amesema Gareth Bale anaweza kuwa bora kama ilivyo kwa Lionel Messi na Cristiano Ronaldo. Bale Hajawahi kumfunga Begovic katika mechi tano walizokutana na golikipa huyo ana matumaini ya kumzuia tena nyota huyo wa kimataifa wa Wales kufunga katika mchezo baina yao wa kufuzu michuano ya Ulaya mwaka 2016 utakaofanyika jijini Cardiff. Begovic mwenye umri wa miaka 27 anayekipiga katika klabu ya Stoke City amesema Messi nap engine Ronaldo ndio wachezaji wawili bora kabisa duniani kwa sasa lakini mchezaji kama Bale anaweza kufikia kiwango hiko kutokana na uwezo wake. Kocha wa timu ya taifa ya Wales, Chris Coleman anaamini Bale ana weza kuifikia rekodi ya kufunga mabao mengine zaidi iliyowekwa na nguli Ian Rush aliyefunga mabao 28 katika mechi 78 alizoitumikia nchi hiyo. Bale mpaka sasa ameshafunga mabao 14 ambapo 11 kati ya hayo amefunga katika mechi 16 zilizopita alizoichezea Wales.

No comments:

Post a Comment