NYOTA wa zamani wa klabu ya Manchester United, Roy Keane ameeleza tabia ya meneja wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho kuwa haikubaliki na kudai kuwa anaweza kusababisha matatizo kama ni mahali pengine. Keane ambaye ni kopcha msaidizi wa klabu ya Aston Villa alionekana katika kamera za video akionyesha kutofurahishwa wakati Mourinho alimfuata yeye na kocha mkuu Paul Lambert muda mfupi kabla mchezo haujamalizika ambapo Chelsea walishinda mabao 3-0 katika uwanja wa Stamford Bridge. Sio jambo geni kwa Mourinho kucheza na akili za mameneja wenzake na mara zote amekuwa akiwahi kushikana mikono na wenzake kabla ya kipenga cha mwisho huku akiondoka uwanjani mchezo ukiwa bado unaendelea. Akizungumza katika uzinduzi wa kitabu chake kipya kiitwacho The Second Half jijini Dublin jana, Keane amesema tabia hiyo ya Mourinho ni ukosefu wa heshima. Keane amesema huwa hajali sana mbinu zake za kuwakejeli mameneja wenzake lakini katika suala la kushikana mikono na wenzake kabla ya mchezo haujamalizika hilo ni suala la ukosefu wa heshima.

No comments:
Post a Comment