TIMU ya mashindano ya langalanga ya Marussia itashindanisha gari moja mwishoni mwa wiki hii katika mashindano ya Grand Prix ya Urusi kwa ajili ya heshima ya dereva wake Jules Bianchi. Dereva huyo raia wa Ufaransa kwasasa anaendelea vyema ingawa bado yuko chini ya uangalizi maalumu kutokana na majeraha ya kichwa aliyopata katika ajali ya mashindano hayo nchini Japan. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Marussia imedai kuwa kutumia gari moja litakaloendeshwa na dereva Max Chilton itakuwa ni hatua muafaka katika kipindi hicho kigumu kinachowakabili. Timu hiyo tayari imeshatengeneza gari lingine ambalo litabakia katika gereji ya Bianchi muda wote wa mashindano ya mwishoni mwa wiki hii.

No comments:
Post a Comment