Friday, October 10, 2014

CAPELLO AKIRI KUKOSEKANA KWA IBRAHIMOVIC ILIKUWA AHUENI KWA URUSI.

KOCHA wa timu ya taifa ya Urusi, Fabio Capello anaamini Zlatan Ibrahimovic angeweza kuleta tofauti kutokana na sare ya bao 1-1 waliyopata dhidi ya Sweden katika mchezo wa kufuzu michuanop ya Ulaya mwaka 2016 uliochezwa jijini Stockholm. Majeruhi yanayomkabili mshambuliaji huyo wa Paris Saint-Germain yamfanya kuukosa mchezo huo wakati Sweden wakipambana kurejesha bao la kujifunga wenyewe na kuhakikisha wanapata sare hiyo. Hata hivyo, Capello amekiri kushukuru kikosi chake hakijakutana na mshambuliaji huyo ambaye ndiye anaongoza nchini humo kwa kufunga mabao mengi zaidi. Capello aliuambioa mtandao wa UEFA kuwa anamfahamu vyema Ibrahimovic na athari zake kwani ni mmoja kati ya wachezaji watatu bora zaidi duniani mwenye uwezo wa kubadili mchezo, kufunga na kutengeneza nafasi. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa mara anapokuwa uwanjani mabeki wa upainzani huwa katika matatizo kutokana na uwezo wake.

No comments:

Post a Comment