Wednesday, October 8, 2014

BAADHI YA MECHI ZA LIGI KUU KUCHEZWA NJE YA UINGEREZA.

KWA mara nyingine Ligi Kuu nchini Uingereza inafikiria wazo la kucheza baadhi ya mechi zao nje ya nchi hiyo. Dhana ya kucheza mechi 39 iliondolewa mwaka 2008 kufuatia utata na upinzani mkali uliojitokeza. Lakini vilabu sasa vinaelekea kukubali kucheza baadhi hizohizo 38 za mzunguko wa ligi zilizokuwepo kuchezwa nje ya nchi. Mazungumzo bado yanaendelea lakini mapendekezo hayo yanaweza kuzaa matunda katika miaka 10 ijayo. Vilabu vikubwa nchini Uingereza vinataka kuongeza umaarufu wa ligi hiyo nje ya nchi kufuatia mahudhurio makubwa katika mechi za kirafiki walizocheza nchini Marekani kiangazi hiki ambapo mchezo wa Manchester United dhidi ya mabingwa wa Ulaya Real Madrid uliochezwa huko Michigan uliingiza mashabiki 109,318. Ligi Kuu pia inashawishika kufanya hivyo kufuatia Ligi ya Mpira wa Kikapu nchini Marekani-NBA na Ligi ya Mpira wa Miguu wa Kimarekani-NFL kucheza baadhi ya mechi zao nchini Uingereza katika msimu ya karibuni.

No comments:

Post a Comment