MENEJA wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson amesisitiza kuwa walikuwa wakielewana vyema na Shinji Kagawa wakati wakiwa wote klabuni hapo lakini pamoja na hayo ameunga mkono uamuzi wa kiungo huyo kurejea katika klabu yake ya zamani ya Borussia Dortmund. Ferguson alimsajili kiungo huyo wa kimataifa wa Japan kutoka Dortmund katika kipindi cha usajili wa kingazi mwaka 2012 na pamoja na kuonyesha uwezo wake kiasi wakati wa msimu wake wa kwanza Old Trafford, Kagawa alishindwa kabisa kuingia katika mipango ya David Moyes wakati Ferguson alipoondoka kabla ya kuamua kurejea Dortmund. Ferguson amesema hajawahi kupoteza imani juu ya uwezo wa Kagawa kung’aa katika Ligi Kuu lakini anaamini nafasi ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 iliingia matata muda mfupi baada ya kusajiliwa kwa Juan Mata kutoka Chelsea Januari mwaka jana. Kocha huyo mkongwe aliendelea kudai kuwa alikuwa na furaha alipokuwa na Kagawa kwani alizoea mapema mazingira lakini kila kocha ana mbinu zake na Moyes alipomnunua Mata, nyota huyo aliona kama sio chaguo la kwanza tena ndio maana anaona alifanya uamuzi sahihi wa kurejea mahali ambapo atajisikia nyumbani.

No comments:
Post a Comment