TAASISI ya Kupambana na Matumizi ya Dawa za Kuonngeza Nguvu Michezoni-WADA inafikiria kuongeza adhabu ya kuwafungia muda mrefu wanariadha ambao wametumia dawa hizo zilizopigwa marufuku kama utafiti utaonyesha dawa hizo kukaa mwilini muda mrefu. Utafiti unaofanywa kupitia panya jijini Oslo unaonyesha baadhi ya madawa yanaweza kuwasaidia wanariadha hata baada ya kumaliza adhabu zao za kufungiwa. WADA walipokea matokeo ya utafiti huo kutoka kwa profesa wa fiziolojia Kristian Gundersen wa Chuo Kikuu cha Oslo lakini mkurugenzi wa masuala ya sayansi wa taasisi hiyo amesema wanahitaji ushahidi kama utafiti huo unaweza kufanya kazi kwa binadamu. Utafiti unaonyesha misuli inaweza kuendelea kunufaika na dawa hizo kwa miaka 10 toka mtumiaji alipoanza kutumia. Kama utafiti huo ukithibitishwa, wanariadha wlaiowahi kufungiwa katika miaka ya karibuni wakiwemo Justin Gatlin na Tyson gay wa Marekani na Mwingereza Dwain Chambers wanaweza kuwa matatani tena. Katika kipindi hiki cha kiangazi, Gatlin mwenye umri wa miaka 32 alikimbia kwa muda wa haraka zaidi katika mbio za mita 100 na 200 pamoja kutumikia adhabu ya kufungiwa mara mbili.

No comments:
Post a Comment