Tuesday, October 21, 2014

BALOTELLI HAPASWI KUCHEZESHWA MECHI YA MADRID - CARRAGHER.

MCHEZAJI mkongwe wa zamani wa Liverpool, Jamie Carragher amesema mshambuliaji nyota wa timu hiyo Mario Balotelli anapaswa kuachwa na badala yake achukuliwe Raheem Sterling kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid. Mshambuliaji huyo wa zamani wa AC Milan amekuwa na msimu mgumu toka asajiliwe kwa kitita cha euro milioni 20 na kukosa nafasi katika mchezo wa Jumapili iliyopita dhidi ya Queens Park Rangers. Kutokana na umuhimu wa mchezo wao huo wa kesho utakaochezwa Anfield, Garragher anadhani kuwa meneja wa klabu hiyo Brendan Rodgers hapaswi kuhatarisha kwa kumpanga Balotelli kwasasa yuko katika kiwango cha chini. Carragher amesema Balotelli hazunguki vya kutosha uwanjani hivyo katika mchezo na timu kama Madrid unahitaji aina ya wachezaji wenye nguvu na wanaocheza kwa juhudi na sio kutembea uwanjani.

No comments:

Post a Comment