Tuesday, October 21, 2014

TAARABT AMPASHA REDKNAPP KUWA YEYE SIO KIBONGE.

KIUNGO wa Queens Park Rangers-QPR, Adel Taarabt amemjibu meneja wake Harry Redknapp ambaye amedai kuwa mchezaji huyo ameongezeka uzito na hakuwa fiti kwa ajili ya kucheza. Kauli hiyo ya Redknapp imekuja kufuatia kipigo cha mabao 3-2 walichopata kutoka kwa Liverpool wakati akiulizwa kwanini kiungo wa kimataifa wa Morocco hakuwemo katika kikosi chake. Taarabt aliuambia mtandao wa Daily Mail kuwa halikuwa jambo la kweli kusema hakuwa fiti kwani anaona alikuwa akitafuta sababu. Kiungo aliendelea kudai kuwa alikuwa na hamu kubwa ya kucheza kabla ya mchezo na alichukizwa kwa kutochezeshwa. Taarabt amesema anashangaa jinsi kocha huyo aliposhindwa kufafanua suala hilo kutokana na uzoefu wake na kuamua kuongea uongo.

No comments:

Post a Comment