CAPE Verde imekuwa nchi ya kwanza kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika-AFCON mwakani baada ya kuitandika Msumbiji kwa bao 1-0 baada ya kupita siku ya nne ya mechi za kufuzu. Algeria ndio waliofuatia baada ya kuizamisha Malawi kwa mabao 3-0 na kuweka rekodi ya kuwa timu pekee iliyovuna alama zote katika michezo minne ya kundi B waliyocheza. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-RDC iliishangaza Ivory Coast kwa kuitandika mabao 4-3 jijini Abidjan wakati mabingwa watetezi Nigeria nao walizinduka na kufufua matumaini yao kufuzu baada ya kuitandika Sudan kwa mabao 3-1 huku Ghana nao wakijiweka katika nafasi nzuri baada ya kupata ushindi mnono wa mabao 3-1 dhidi ya Guinea. Angola, Cameroon, Misri, Ethiopia, Togo na Tunisia wote walishinda mechi zao wakati mechi kati ya Afrika Kusini dhidi ya Congo Brazaville na Burkina Faso dhidi ya Gabon zote zilimalizika kwa sare.

No comments:
Post a Comment