MENEJA wa zamani wa klabu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson amedai kuwa Louis van Gaal anafanya sahihi kutengeneza kikosi chake mwenyewe Old Trafford. Akihojiwa na luninga ya MUTV, Ferguson aliunga mkono mpango huo wa Van Gaal na kudai kuwa ana uzoefu wa kutosha wa kufanya hivyo. Van gaal alitumia zaidi ya paundi milioni 150 wakati wa kipindi cha usajili wa majira ya kiangazi ukiwemo usajili uliovunja rekodi nchini Uingereza wa paundi milioni 59.7 kwa ajili ya kiungo Angel Di Maria. Kocha huyo pia amewaacha wachezaji 14 akiwemo Danny Welbeck aliyekwenda Arsenal kwa kitita cha paundi milioni 16 toka alipotua hapo Julai mwaka huu. Ferguson alistaafu Mei mwaka jana na kumuachia nafasi yake David Moyes ambaye naye alidumu kwa kipindi miezi 10 pekee kabla ya kuingia Van Gaal.

No comments:
Post a Comment