WAKALA wa mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Ureno, Cristiano Ronaldo amedai kuwa nyota huyo hana mpango wowote wa kurejea Manchester United na anatarajia kutundika daruga zake akiwa Real Madrid. Ronaldo mwenye umri wa miaka 29 tayari amefunga mabao 15 msimu huu ikiwemo hat-trick yake ya 22 katika La Liga. Kumekuwa na tetesi zinzomhusisha Ronaldo na kurejea katika klabu yake ya zamani ya United lakini taarifa hizo zimekanushwa na wakala wake Jorge Mendez. Mendez amesema Ronaldo ana furaha Madrid na ataendelea kuvunja rekodi zote na kustaafu akiwa hapoi. Wakala huyo aliendelea kudai kuwa haitawezekana kutokea mchezaji wa aina yake kwa mingi sana ijayo kwa kila siku anazidi kuimarika na atendelea hivyo mpaka atakapofikia miaka 40. Ronaldo aliondoka United kwenda Madrid mwaka 2009 kwa kitita cha paundi milioni 80.

No comments:
Post a Comment