Thursday, October 2, 2014

HATIMAYE FIFA YAKUBALI UCHAGUZI WA NFF.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA wiki hii limeutambua uchaguzi wa Shirikisho la Soka la Nigeria-NFF na kudai kutuma barua ya kumpongeza rais mpya Amaju Pinnick. FIFA sasa inaweza kuondoa vitisho vya kuifungia nchi hiyo ambao ni mabingwa wa Afrika kufuatia miezi kadhaa ya mvutano na tuhuma za serikali kuingilia masuala ya NFF ambayo kisheria hairuhusiwi. Nigeria ilifungiwa kwa siku tisa Julai mwaka huu baada ya rais aliyemaliza muda wake Aminu Maigari kukamatwa wakati akirejea kutoka katika Kombe la Dunia na wizara ya michezo ya nchi hiyo kumteua kiongozi mwingine kuongoza. Adhabu hiyo iliondolewa baada ya Maigari kurejeshewa wadhifa wake huo lakini waliingia katika vitisho vingine vya kufungiwa mwezi uliopita wakati Maigari alipoondolewa katika kiti chake hicho kwa mara ya pili katika uchaguzi ambao haukutambuliwa na FIFA. Sasa mambo yanaonekana kupoa NFF baada ya uachaguzi baada ya Pinnick kupokea ujumbe wa pongezi kutoka kwa rais wa FIFA Sepp Blatter huku serikali ya nchi hiyo ikionywa kutoingilia tena masuala ya soka na katibu mkuu waFIFA Jerome Valcke.

No comments:

Post a Comment