MSHAMBULIAJI mkongwe wa kimataifa wa Uholanzi, Dirk Kuyt ameamua kustaafu soka la kimataifa baada ya kutumikia nchi yake kwa mechi 104. Nyota huyo anayekipiga katika klabu ya Fenarbahce alikuwa sehemu ya kikosi cha Uholanzi kilichomaliza katika nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu nchini Brazil chini ya kocha aliyeondoka Louis van Gaal. Kuyt pia aliitwa katika kikosi hicho na kocha mpya Guus Hiddink katika michezo mwili iliyochezwa mwezi uliopita dhidi ya Italia na Jamhuri ya Czech. Akihojiwa Kuyt mwenye umri wa miaka 34 amesema amapata wakati mgumu kuchukua uamuzi huo lakini anadhani wakati wake umefika wa kutoa nafasi kwa wengine wanaochipukia kulitumikia taifa hilo. Kuyt aliendelea kudai kuwa atakumbuka kila kitu na imekuwa heshima kubwa kwake kulitumikia taifa hilo kwa kipindi chote. Nyota huyo alipewa nafasi kwa mara ya kwanza kukitumikia kikosi cha Uholanzi na kocha Marco van Basten katika mchezo dhidi ya Liechtenstein mwaka 2004.
No comments:
Post a Comment