KLABU kongwe nchini Misri ya Zamalek imemtimua kocha wake Hossam Hassan ikiwa imepita miezi michache toka walipomteua kama kocha mkuu. Zamalek ilimchukua Hassan baada ya kumtimua kocha wao wa zamani Ahmed Hossam Mido Julai mwaka huu. Bodi ya klabu hiyo chini ya kiongozi wao Mortada Mansour iliitisha mkutano na kuamua kumtimua kocha huyo sambamba na pacha wake Ibrahim ambaye alikuwa akifanya kazi kama mkurugenzi wa timu katika benchi lao la ufundi. Bodi hiyo pia iliamua kumteua Mohamed Salah kuwa kocha wa muda wa michakato ya kutafuta kocha mwingine ikifanyika. Uamuzi wa kumtimua Hassan umekuja kufuatia matokeo mabaya ambayo imekuwa ikipata timu hiyo katika mechi za hivi karibuni za Ligi Kuu ya nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment