Friday, October 3, 2014

RAMIRES ATEMWA BRAZIL.

SHIRIKISHO la Soka nchini Brazil-CBF limedai kuwa limemtema kiungo wa Chelsea Ramires katika kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Argentina na Japan na nafasi yake itachukuliwa na Souza anayecheza klabu ya Sao Paulo. CBF imedai kuwa Souza mwenye umri wa miaka 25 ambaye ni kiungo wa ulinzi ataungana na mchezaji mwingine ambaye ameitwa kwa mara ya kwanza golikipa wa Gremio Marcelo Grohe. Ramires ameachwa kutokana na kusumbuliwa na matatizo ya misuli. Grohe, ambaye hajafungwa katika mechi nane mfululizo akiwa na Gremio, amechukuliwa kama tahadhari baada ya golikipa chaguo ka kwanza Jefferson kuumia kidole wakati akiitumikia klabu yake ya Botafogo. Brazil itakwaana na Argentina jijini Beijing Octoba 11 na baadae kuivaa Japan nchini Singapore siku tatu baadae.

No comments:

Post a Comment