Friday, October 3, 2014

SUAREZ AITWA URUGUAY.

KOCHA wa timu ya taifa ya Uruguay, Oscar Tabarez amemjumuisha Luis Suarez katika kikosi chake cha wachezaji 22 aliowaita kwa ajili ya michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa mwezi huu dhidi ya Saudi Arabia na Oman. Hiyo inakuwa mara ya kwanza kwa nyota huyo kuitwa katika kikosi hicho toka alipomng’ata beki wa kimataifa wa Italia Giorgio Chiellini katika michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil. Ingawa ameruhusiwa kucheza mechi za kirafiki, Suarez bado anaendelea kuitumikia adhabu ya mechi tisa za mashindano alizofungiwa hatua ambayo inamaanisha ataikosa michuano ya Copa Amerika na baadhi ya mechi za kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2018. Adhabu hiyo pia inajumuisha mechi za mashindano za klabu yake ya Barcelona ambayo ataimaliza baadae mwezi huu.

No comments:

Post a Comment