MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Danny Welbeck amewakosoa waajiri wake wa zamani Manchester United kwa kusisitiza kuwa walikwamisha kiwango chake kwa kumchezesha kama winga wakati akiwa huko. Mameneja wa United akiwemo Sir Alex Ferguson, David Moyes na Louis van Gaal wote walimtumia Welbeck kama mshambuliaji wa pembeni huku Van Gaal akifafanua hivi karibuni kuwa nyota huyo hakufunga mabao ya kutosha. Lakini Welbeck amekuwa katika kiwango cha juu toka alipohamia Arsenal kwa kitita cha paundi milioni 16 na sasa amefunga mabao manne katika mechi tano alizocheza baada ya kufunga mabao matatu au hat-trick katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Galatasaray. Akihojiwa Welbeck amesema hakuna yoyote anayeweza kumkosa moja kwa moja kwasababu hawajawahi kumuona akicheza katika ya ushambuliaji wa kati mara kwa mara. Welbeck aliendelea kudai kuwa sasa anapata nafasi hiyo na anachofanya ni kutumbukiza mipira katika wavu kama ilivyo kwa washambuliaji wengine.
No comments:
Post a Comment