Friday, October 3, 2014

FABREGAS ALITAKA KURUDI ARSENAL - WENGER.

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amedai kuwa Cesc Fabregas alitaka kujiunga nao tena kabla ya kujiunga na Chelsea. Nahodha huyo wa zamani wa Arsenal aliwahi kuitumikia timu hiyo kwa miaka nane kabla ya kuhamia Barcelona lakini baada ya kushindwa kutamba alihamia Stamford Bridge kwa kitita cha euri milioni 36 katika usajili wa kiangazi. Pamoja na kwenda kwa mahsimu wao Wenger ameonyesha bado kumkubali kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania. Wakati akiulizwa kama Fabregas alitaka kurejea Arsenal, Wenger alikubali na kudai kuwa pamoja na kwamba hakuzungumza naye moja kwa moja lakini alitaarifiwa kuwa anaweza kwenda Chelsea. Wenger aliendelea kudai kuwa wakati kiungo alipondoka kwenda Barcelona walimnunua Mesut Ozil hivyo hawakuwa na haja ya kusajili kiungo wa kushambulia katika usajili wa kiangazi. Pamoja na hayo Wenger amesema bado anampenda nyota huyo na kuheshimu maamuzi yake na kudai kuwa anastahili kupokewa kwa heshima pindi timu hizo zitakapokutana Jumapili.

No comments:

Post a Comment